Tshisekedi aiwekea masharti serikali ya DRC | Matukio ya Afrika | DW | 01.08.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Tshisekedi aiwekea masharti serikali ya DRC

Kiongozi wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Etienne Tshisekedi, anataka uchaguzi mkuu ufanyike kabla ya Desemba 20 mwaka huu na wafungwa wa kisiasa waachiwe huru kabla ya mazungumzo ya kitaifa.

Sikiliza sauti 02:37

Ripoti ya Saleh Mwanamilongo kutoka Kinshasa

Maelfu ya wafuasi wa vyama vyote vya upinzani nchini DRC walijitokeza toka asubuhi mapema ya Jumapili kwa ajili ya hotuba wa Etienne Tshisekedi. Ni hotuba yake ya kwanza mjini Kinshasa toka uchaguzi wa mwaka 2011. Junior Mutala mwenye umri wa miaka 21 amesema hotuba wa Etienne Tshisekedi imempa imani ya mageuzi ya kidemokrasia nchini. "Kila siku wametuambia kuhusu mazungumzo ya kitaifa, leo tumepata ufafanuzi kwamba mazungumzo hayo yanatakiwa kuheshimu katiba ya Kongo. Na muhula wa pili wa Kabila hauna uhusiano wowote na mazungumzo bali anatakiwa kuheshimu katiba."

Wafuasi wa upinzani wakiandamana Kinshasa

Wafuasi wa upinzani wakiandamana Kinshasa

Akizungukwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, Etienne Tshisekedi alilazimisha kuweko na uchaguzi wa Rais kabla ya mwaka huu kumalizika: "Tarehe 19 Septemba itakuwa ni angalisho la kwanza kwa tume ya uchaguzi na Rais Kabila kwani tume ya uchaguzi inatakiwa kuandaa uchaguzi siku 90 kabla ya muhula wa rais kumalizika. Ikiwa hawatafikia hilo watatakiwa kujiuzulu."
Wapiga kura waandikishwa

Kinara wa upinzani nchini DRC alielezea kwamba upinzani uko tayari kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa, lakini bila msuluhishi aliyeko hivi sasa. "Edem Kodjo ni mtu wa Kabila na amefanya kazi kwa ajili ya Kabila. Wananchi hawawezi kumpa imani yao ili kusuluhisha mazungumzo hayo. Tunaomba muungano wa Afrika kuteuwa mtu mwingine."

Baada ya mkutano huo, mbunge Gregoire Lusenge amesema vyama vya upinzani vinatafakari hatua itakayofuata. Etienne Tshisekedi alielezea pia umuhimu wa kuachiliwa huru wafungwa wote wa kisiasa na kuomba kutupiliwa mbali kwa kesi dhidi ya Moise Katumbi kabla ya mazungumzo ya kitaifa. Wakati huo huo, tume huru ya uchaguzi Ceni imeanzisha operesheni ya kuandikisha wapiga kura. Operesheni hiyo itakayodumu kwa miezi kumi ilianzishwa jimboni Nord-Ubangi, Kasakzini Magharibi mwa Kongo.


Sauti na Vidio Kuhusu Mada