1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump na washirika wake huenda walitenda uhalifu

Bruce Amani
3 Machi 2022

Jopo la bunge linalochunguza uasi wa Januari 6 kwenye majengo ya Bunge la Marekani kwa mara ya kwanza limesema kuwa ushahidi wake unaashiria uhalifu huenda ulifanywa na Rais wa zamani Donald Trump

https://p.dw.com/p/47wrg
USA I Ex-Präsident Donald Trump startet neuen Wahlkampf
Picha: Gaelen Morse/REUTERS

Jopo hilo limesema Trump na washirika wake huenda walifanya uhalifu huo katika jaribio lililoshindwa la kuyabatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa 2020. 

Kamati ya bunge imesema katika ripoti yake kwa mahakama kuwa Trump na wale waliofanya kazi naye walisambaza habari za uwongo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais na kuwashinikiza maafisa wa majimbo kuyabatilisha matokeo, na hivyo kuwa na uwezekano wa kukiuka sheria kadhaa za nchi. 

Wabunge wa Marekani hawana mamlaka ya kuwasilisha mashitaka ya uhalifu wao wenyewe na wanaweza tu kufanya hivyo kupitia kwa Wizara ya Sheria.

Wizara hiyo imekuwa ikichunguza vurugu hizo za mwaka jana lakini haijatoa ishara yoyote kuwa inazingatia kumfungulia Trump mashitaka. 

Chanzo: afp