Trump kukutana na viongozi wa Rwanda na Kongo Alhamis
2 Desemba 2025
Matangazo
Mkutano huo unatarajiwa kuboresha makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani mwezi Juni na kutiwa saini na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili, pamoja na mpango mkakati wa kiuchumi ulioafikiwa mwezi Novemba. Wakati hatua hiyo ikitarajiwa kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda lilifanya mashambulizi ya kushtukiza mashariki mwa Kongo mwaka huu, likiteka miji mikuu miwili ya eneo hilo na kuzua hofu ya vita vikubwa zaidi.