1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump awasili Saudi Arabia

Sekione Kitojo
21 Mei 2017

Rais Donald Trump  akikaribishwa  kwa bashasha  kubwa  na  ukoo  wa  kifalme  wa  Saudi Arabia, wakati  akiweka  kando, japokuwa  kwa  muda  tu , utata mkubwa  unaoukumba utawala  wake  mjini  Washington.

https://p.dw.com/p/2dJ8h
Saudi Arabien - Donald Trump zu Besuch in Riad
Rais Trump akilakiwa mjini RiyadhPicha: picture-alliance/dpa/AP/E. Vucci

Trump  amewazawadia  wenyeji wake  mpango  wa mauzo  ya  bilioni 110  wa  silaha  wenye  lengo  la  kuimarisha  usalama  wa  Saudi  Arabia pamoja  na  makubaliano  kadhaa  ya  kibishara.

"Hii  ni  siku  muhimu  sana, uwekezaji  mkubwa  katika  Marekani ," Trump  alisema wakati wa  mkutano  na  mwanamfalme Mohammed bin Nayef.

Auslandreise US-Präsident Trump in Saudi-Arabien
Rais Trump (Kushoto) akisalimiana na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz(kulia)Picha: Getty Images/AFP/M. Ngan

Ziara  katika  mji  mkuu  wa  Saudi Arabia  ilikuwa  ni ziara  ya  kwanza  ya  Trump  nje  ya nchi  akiwa  rais, ikiwa  ni  ziara  itakayokuwa  na vituo  vitano ambayo  itamchukua  katika mataifa  ya  mashariki  ya  kati  hadi  Ulaya. Ni  rais  pekee  wa  Marekani kuifanya  Saudi Arabia , ama  taifa  lolote  lenye  Waislamu  wengi kuwa  kituo  chake  cha  kwanza  nje  ya nchi.

Trump  aliwasili  mjini  Riyadh akizongwa  na  hatua  yake  ya  kumfuta  kazi  mkurugenzi  wa FBI James Comey  na  hali  ya  kufichuka zaidi  juu  ya  uchunguzi  wa  serikali  kuu kuhusiana  na  uwezekano  wa  mahusiano  ya kampeni  na  Urusi.

Akikimbia  mambo  mjini Washington  na  kukumbatiwa  na  familia  ya  kifalme inaonekana kumpa  nguvu  Trump.

Melania  hakufunika nywele

Baada  ya  safari  ya  usiku  kucha , rais  alilakiwa  katika  uwanja  wa  ndege  na  Mfalme Salman , hali  iliyoonekana kuwa  ni  ya  aina  ya  kipekee  kwa  kuwa  mfalme  hakuonekana mwaka  jana  wakati  wa  kumlaki rais Barack Obama  katika  ziara  yake  ya  mwisho  nchini Saudi  Arabia.

Saudi Arabien US-Präsident Trump und König Salman bin Abdulaziz al-Saud unterzeichnen Verträge
Rais Trump akitia saini makubaliano ya mauzo ya silaha pamoja na mfalme Salman bin Abdulaziz al-SaudPicha: Getty Images/AFP/M. Ngan

Trump  aliongozana  katika  ziara  yake  hiyo  na  mkewe Melania  Trump, ambaye  alivalia suti  nyeusi na  mkanda  wa  dhahabu, lakini  hakufunika  nywele  zake  katika  nchi  hiyo  ya kifalme  ambayo ni  ya  kihafidhina  zaidi, kwa  mujibu  wa  utamaduni  wa  ujumbe  wa kimagharibi.

Mapokezi  makubwa  ya  Trump  yanaakisi  kiwango  ambacho  Saudi  Arabia  imekuwa hairidhishwi  na  Obama. Wasaudi  kwa  kiasi  kikubwa  hawakumuamini  Obama  kuhusiana na  mahusiano  yake  na  Iran na  wamekasirishwa  na  mtazamo  wake  wa  kujizuwia kuhusiana  na  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe  nchini  Syria.

Auslandreise US-Präsident Trump in Saudi-Arabien - Melania Trump
Mke wa rais wa Marekani Melania Trump(kushoto) akiwa pamoja na mwanamfalme Muhammad nin nayef bin Abdulaziz al-SaudPicha: Getty Images/AFP/M. Ngan

Wairani wachagua rais

Wakati  Trump  anawasili , Wairani  walikuwa  wamemchagua  tayari  Hassan Rouhani , mmoja  kati  ya  washirika  wa  Obama   katika  makubaliano  ya  kihistoria  yaliyokuwa  na lengo  la  kudhibiti  nia  ya  Iran  ya  kujipatia  silaha  za  kinyuklia, kwa  muhula  wa  pili  wa miaka  minne kuwa  rais, akielezea  msukumo  wake  kwa  ajili  ya  uhuru  zaidi  na kuzijongelea  zaidi  nchi  nyingine  duniani.

Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Marekani  Rex Tillerson  amesema  ana  matumaini Rouhani  atatumia  kipindi chake  hicho  kipya  madarakani  "kuanza  mchakato  wa kuvunjilia  mbali  mtandao  wa kigaidi  wa  Iran."

Donald Trump, Melania Trump, König Salman
Rais Trump akiwasili katika kasri la mfalme wa Saudi Arabia Picha: picture alliance/AP Photo/E.Vucci

Trump  hakutoa  matamshi yeyote  katika  siku  yake  ya  kwanza  nje  ya  nchi  na  alitumia muda  wake  mwingi  akitembea  kati ya  vyumba  mbali  mbali  vya  kasri  la  mfalme.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / ape

Mhariri: Sudi Mnette