1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump anatarajia kukamatwa Jumanne

Angela Mdungu
18 Machi 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema anatarajia kukamatwa na polisi Jumanne, katika kesi iliyofikishwa kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa Manhattan Alvin Bragg

https://p.dw.com/p/4Ot0p
USA Donald Trump Davenport
Picha: Scott Olson/Getty Images

Trump, ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Truth social bila kutaja tuhuma zitakazosababisha akamatwe huku akiituhumu ofisi ya mwanasheria mkuu wa mji wa Manhattan kuwa iliyojaa rushwa.

Rais huyo wa zamani wa Marekani amewataka wafuasi wake waandamane kupinga hatua hiyo.

Soma zaidi Wabunge Marekani wataka Trump ashtakiwe

Ofisi ya Bragg mapema mwaka huu ilianza kuwasilisha ushahidi kwa jopo la majaji ili kuchunguza malipo ya dola za kimarekani 130,000 yaliyofanywa na mwanasheria binafsi wa zamani wa Trump Michael Cohen kwenda kwa mcheza filamu za ngono Stormy Daniels katika siku za mwisho za kampeni  mwaka 2016.