1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump afuta misaada kwa wanaotoa mimba

2 Februari 2017

Maelfu ya wanawake watafariki dunia kutokana na utoaji mimba usio salama. Yote hayo yatatokana na uamuzi wa Rais Donald Trump kufuta ufadhili wa Marekani kwa makundi yanayosaidia wanawake kutoa mimba.

https://p.dw.com/p/2WraF
USA | Pro-life und Pro-Choice activists auf dem National March for Life Washington
Picha: REUTERS/A. P. Bernstein

Hatua ya Rais Trump itayaathiri mashirika ya Kimarekani yanayotoa misaada nchi za nje. Lakini  upinzani wake dhidi ya utoaji mimba litakuwa ni jambo gumu kulifuatilia kisheria katika nchi nyingi zinazoendelea, kwa sababu sheria ziliopo,unyanyapaa na umasikini. Mwanaharakati Rosemarry Olale kutoka Kenya ambaye husaidia kuwafunza wasichana katika  maeneo ya  wakaazi masikini  mno mjini Nairobi, juu ya elimu ya uzazi,anasema  wanawake watalazimika kutafuta njia nyengine kutoa mimba ambazo hazitakua za usalama.

Taifa hilo la Afrika mashariki   ni miongoni mwa zile zenye kiwango cha juu cha utoaji mimba duniani na nyingi huwa si salama, zikisababisha  majeraha na mauti  miongoni mwa wanawake. Kwa mujibu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, kuna wanawake 21.6 milioni duniani kote ambao hutoa mimba  kwa njia zisizo salama kila mwaka na  9 kati  ya 10 hufanyika katika nchi zinazoendelea.

Utoaji mimba hatari kuongezeka

Mwanafunzi aliyetoa mimba Tanzania
Mwanafunzi aliyetoa mimba Tanzania Picha: DW/K. Makoye

Mashirika  yanayosaidia wanawake kutoa mimba na kuhakikisha wako salama, ni pamoja na  Shirikisho la kimataifa libnalojulikana kama  Planned Parenthood Federation na Marie Stopes, ambayo ni miongoni mwa yatakayoathirika kutokana na  uamuzi wa Trump kupiga marufuku ufadhili wa mashirika  yanayosaidia  wanawake katika hilo.  Maafisa wa mashirika hayo mawili wanasema bila ya ufadhili , kutakuweko na utoaji mimba milioni 2.1 katika njia zisizo salama na  vifo 71,700 kutokana na uzazi, katika kipindi cha kwanza cha utawala wa Trump, jambo ambalo kimsingi linaweza kuzuiwa na kuepusha athari na maisha ya  wanawake.

Shirika la  Marie Stopes limekuwa likipokea dola milioni 30  kila mwaka kutoka  Shirika  la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa ajili  ya  kuwasaidia  wanawake  juu ya  huduma za mipango ya familia. milioni moja na nusu katika zaidi ya nchi 12. Sasa  huduma hizo zitabidi zipunguzwe, ikiwa fedha hazitopatikana.

Sheria inayojirudia

Donald Trump alisaini amri ya rais ya kufuta ufadhili wa Marekani kwa mashirika yanayowapa wanawake nafasi kutoa mimba au kuwashauri kuhusu swala hilo.
Donald Trump alisaini amri ya rais ya kufuta ufadhili wa Marekani kwa mashirika yanayowapa wanawake nafasi kutoa mimba au kuwashauri kuhusu swala hilo. Picha: picture-alliance/CNP/A. Harrer

Wanawake wanaoishi katika maeneo ya  vijijini bila ya huduma za serikali wataathirika zaidi. Afisa  Maaike van Min kutoka  Shirika  hilo la Marie  Stopes  anazitaja miongoni mwazo kuwa ni Nigeria na Madagascar ambako Shirika hilo lina miradi mikubwa .

Mkurugenzi wa Afrika wa  kituo  kinachotetea haki ya uzazi  Evelyne Opondo anakumbusha juu ya  huduma nyingi zilizoathrika  nchini Kenya baada ya  Rais  George W. Bush kuingia madarakani  2001 na kuirejesha sheria ya kupiga marufuku  kufadhili utoaji mimba. Na sasa chini ya  Trump  hatua hiyo  ilioodolewa baada ya Bush kuondoka madarakani , sasa inarudi tena.  Mashirika  husika yakalazimika pia kupunguza huduma kwa  wahanga wa matumizi ya nguvu kingono na  wenye virusi vya Ukimwi (HIV).

Utafiti wa  Shirika la Afya Duniani pamoja na hayo, unasema kiwango cha  utoaji mimba  katika kanda ya  Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara wakati wa  utawala wa Bush kiliongezeka. Bibi Opondo anasema "inasikitisaha kwamba  maisha  na afya za  wanawake zinawekwa reheani, kutokana na  sera za Marekani." Anasema  Huo ni ukosefu wa uadilifu na  kutothamini utu wa binaadamu."

Mwandishi: Saumu Mwasimba (Thomson Reuters Foundation )

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman