1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Mahakama kuu yaidhinisha hukumu ya kifo kwa wauguzi na daktari

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBju

Mahakama kuu ya Libya imethibitisha uamuzi wa hukumu ya kifo katika kesi iliyowakabili wauguzi watano wa Bulgaria na daktari mmoja kutoka Palestina.

Wataalamu hao wa afya walishtakiwa kwa kuwaambukiza ukimwi watoto zaidi ya 400 katika hospitali moja nchini Libya mnamo mwaka wa 1998.

Wauguzi wote watano kutoka Bulgaria na daktari mmoja kutoka Palestina, bado mpaka sasa wanakanusha mashataka hayo wakisema hawana hatia.

Mahakama kuu ilitarajiwa kubatilisha hukumu hiyo ya kifo dhidi ya wauguzi hao, lakini uamuzi wa mwisho ulitarajiwa kupitishwa na baraza kuu la mahakama. Wakfu wa Gaddafi iliyokuwa mpatanishi katika kesi hiyo, ilisema jana kwamba makubaliano ya malipo yaliyokubaliwa na pande zote husika yamefikiwa ili kumaliza mzozo huo.

Kufikia sasa watoto 56 kati ya watoto 438 walioambukizwa ukimwi katika hospitali ya mjini Tripoli mwaka wa 1998 wamefariki dunia. Wauguzi wote walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifo mara mbili mwaka wa 2004 na mwaka jana baada ya kukata rufaa.