1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Juhudi zaidi zaendelea kutafuta suluhisho la mzozo wa Darfur

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCL7

Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan, Andrew Natsios amewasili mjini Tripoli Libya hii leo kwa mazungumzo na wakuu wa huko juu ya mzozo wa Darfur.

Kiongozi wa Libya, Kanali Muhammar Gadaffi, amekwishaanda mikutano kadhaa midogo, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kuzungumzia juu ya vita vya Darfur, ambapo inaarifiwa mpaka sasa vimekwishagharimu maisha ya watu lakini mbili na wengine milioni mbili unusu kuyakimbia makazi yao toka mwaka 2003.

Kanali Gaddafi ambaye anapigia upatu matatizo ya afrika kutatuliwa na waafrika wenyewe na kuachana na diplomasia ya nchi za magharibi, anachukuliwa kama rafiki mkubwa wa majirani zake Sudan na Chard.