1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tripoli. Blair aifagilia Libya.

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwj

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair , ambaye anaizuru Libya , amekutana na kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

Baadaye , Blair aliwaambia waandishi wa habari kuwa uhusiano baina ya mataifa hayo mawili umebadilika kabisa katika muda wa miaka mitatu iliyopita.

Hapo mapema , Blair ameisifu nchi hiyo ambayo hapo zamani ilikuwa imetengwa kimataifa , kutokana na ushiriki na usaidizi wake katika kupambana na ugaidi.

Mataifa hayo mawili yametangaza makubaliano kadha ya nishati na ulinzi ikiwa ni pamoja na mauzo ya makombora kutoka Uingereza na mfumo wa ulinzi wa anga.

Libya ilikumbana na vikwazo vya kimataifa hadi mwaka 2004 wakati ilipoacha juhudi zake za kujipatia silaha za kinuklia na kukubali kulipa fidia kwa ajili ya shambulio dhidi ya ndege ya abiria mwaka 1988 katika anga ya Lockerbie nchini Scotland , ambapo watu 270 walipoteza maisha yao.