Toulouse:Merkel kukutana na Sarkozy leo | Habari za Ulimwengu | DW | 16.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Toulouse:Merkel kukutana na Sarkozy leo

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel atakutana na rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy kusini mwa Ufaransa leo, kuzungumzia hali ya baadae ya kampuni ya safari za anga ya Ufaransa EADS, inayotengeneza ndege za Airbus. Kampuni hiyo inaongozwa na wenyeviti wa pamoja wa Ujerumani na Ufaransa, ambao wamekua wakikosolewa kwa usimamizi na uendeshaji mbaya. Bibi Merkel amesema kwamba zingatio la biashara halina budi kuchukua nafasi ya usoni kuliko siasa , katika uendeshaji wa kampuni hiyo, wakati Bw Sarkozy anataka usemi zaidi wa serikali. Ripoti za magazeti zimefichua kwamba viongozi hao wawili watatangaza kwamba Meneja wa kampuni hiyo mfaransa Louis Gallois anakua mwenyekiti pekee, wakati mwenyekiti mwenza wa hivi sasa, mjerumani Thomas Enders, atakua mwenyekiti mtendaji wa kitengo cha ndege za Airbus.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com