Toulouse:Mageuzi ya uongozi katika kampuni la safari za anga la ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 16.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Toulouse:Mageuzi ya uongozi katika kampuni la safari za anga la ulaya

Kampuni kubwa ya safari za anga barani Ulaya EADS imetangaza mageuzi ykatika usimamizi na uendeshaji wa pamoja wa kati ya Ufaransa na Ujerumani. Mwenyekiti mwenza , Mfaransa Louis Gallois sasa anakua mkuu mtendaji pekee wa kampuni hiyo wakati mwenzake Mjerumani Thomas Enders atakua mkuu wa kitengo cha ndege aina ya Airbus. Utata katika usimamizi kimetajwa kuwa chanzo cha kushindwa kufanya kazi ipasavyo pamoja na matatizo kadhaa yaliojitokeza. Uamuzi huo umechukuliwa katika mkutano baina ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy leo mjini Toulouse. Sambamba na hayo viongozi hao wanatarajiwa kuzungumzia maswala ya sera ya uchumi ya Ulaya ,yakiwemo matamshi ya Bw Sarkozy hivi karibuni, kupinga kuwa na sarafu ya Euro yenye nguvu akisema ni kikwazo kwa mashindano ya biashara.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com