Tottenham yamtimua kocha Andre Villas Boas | Michezo | DW | 16.12.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Tottenham yamtimua kocha Andre Villas Boas

Na kule London, Klabu ya Tottenham Hotspur imefanya uamuzi wa haraka kutokana na kichapo chao cha mabao matano kwa sifuri walichopewa na Liverpool, kwa kumpiga kalamu leo kocha Andre Villas Boas.

ARCHIV Chelsea trennt sich von Trainer Andre Villas-Boas

Andre Villas Boas amekuwa chini ya shinikizo tangu alipochukua uongozi mwanzoni mwa msimu

Klabu hiyo imesema katika taarifa kuwa uamuzi huo umetokana na “makubaliano na maslahi ya pande zote mbili”. Kichapo dhidi ya Liverpool kimewaweka katika nafasi ya saba kwenye Premier League, point I nane nyuma ya viongozi Arsenal na tano nyuma ya nafasi ya kucheza katika Champions League.

Villas Boas alichukua uongozi mwanzoni mwa msimu, na amekuwa chini ya mbinyo kutoka mwanzo baada ya kutumia kiasi cha zaidi ya pauni milioni 100 kwa kuwasajili wachezaji wapya, ijapokuwa alipata pauni milioni 85 kutoka kwa mauzo ya Gareth Bale aliyehamia Real Madrid. Jana usiku Villas Boas aliahidi kuwa hawezi kung'atuka akisema wachezaji wake watajinyanyua tena haraka na kuendelea kupigania nafasi nzuri.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman