TOKYO: Kansela Merkel akamilisha ziara ya Bara Asia | Habari za Ulimwengu | DW | 31.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOKYO: Kansela Merkel akamilisha ziara ya Bara Asia

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel leo Ijumaa anakamilisha ziara yake nchini Japan.Mjini Kyoto leo mchana,Merkel atatoa hotuba muhimu kuhusu tatizo la kuongezeka kwa kiwango cha joto duniani.

“Itifaki ya Kyoto“ kuhusu njia za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani,ilitiwa saini miaka kumi iliyopita mjini Kyoto.

Kansela Merkel,kutoka Kyoto ataelekea Osaka kuhudhuria Mashindano ya Riadha Ulimwenguni na atarejea Ujerumani siku ya Jumamosi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com