1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOAMASINA:Rajaonarivelo azuiliwa kurejea nyumbani

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4z

Madagaskar imeufunga uwanja wa ndege wa Toamasina mashariki mwa nchi hiyo.Hatua hiyo imechukuliwa ili kumzuia kiongozi wa upinzani alie uhamishoni kurejea nyumbani kabla ya kumalizika wakati wa kujiandikisha kama mgombea urais katika uchaguzi ujao.Licha ya kukabiliwa na kitisho cha kukamatwa,naibu waziri mkuu wa zamani,Pierrot Rajaonarivelo,anaejitayarisha kugombea uchaguzi wa rais mwezi wa Desemba,alitarajiwa kutua katika uwanja huo wa ndege.