1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tishio la ugaidi

30 Oktoba 2010

Rais Obama wa Marekani asema kugunduliwa kwa vifurushi hivyo ni tishio la ugaidi.

https://p.dw.com/p/PuZq
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: AP

Polisi ya Dubai imesema vifurushi vilivyokuwa na miripuko na vilivyokuwa vinasafirishwa kuelekea nchini Marekani, vina ishara ya mkono wa makundi ya kigaidi kama  Al-Qaeda. Taarifa hiyo ya polisi ilisema uchunguzi umebainisha kuwa  vifurushi hivyo kutoka Yemen katika mashine yake moja ya kupigia chapa ya kompyuta wino wake ulikuwa na vitu vya miripuko. Zaidi ilisemekana kifaa hicho cha kuripuka kilitengenezwa kwa ustadi mkubwa kwa kuunganisha waya wa umeme na kadi ya simu ya mkono iliofichwa katika mashine hiyo ya kupiga chapa. Maafisa hao wa polisi waliongeza kusema ustadi wa aina hiyo hutumiwa na makundi kama ya Al-Qaeda.