1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu zatafuta tikiti ya hatua ya mchujo

Bruce Amani
20 Novemba 2017

Dimba la Kombe la Klabu bingwa Ulaya linarejea tena kesho ambapo timu 12 zinapambana kujikatia tikiti ya kutinga hatua ya kwanza ya mchujo

https://p.dw.com/p/2nwoa
Fussball UEFA Champions League - Tottenham vs Real Madrid - Cristiano Ronaldo
Picha: Getty Images/I. Kington

Real Madrid watafuzu kama watashinda dhidi ya Apoel Nicosia katika Kundi H, wakati Totteham wakipambvana na Borussia Dortmund wakifahamu kuwa ushindi utawapa uongozi wa kundi hilo.

Barcelona watatinga 16 za mwisho katika Kundi D kama watatoka sare mjini Turin dhidi ya Juventus ambao wataweza tu kufuzu kwa kutoka sare kama Sporting Lisbon watashindwa kuwaangusha Olympiakos.

Katika Kundi C, Atletico Madrid wanahitaji ushindi dhidi ya wageni Roma katika mechi muhimu ya Jumatano, wakati Chelsea wakitafuta ushindi ili kufuzu dhidi ya Qarabag, mechi ambayo kocha wa Chelsea Antonio Conte ameitaja kuwa muhimu Zaidi kufikia sasa msimu huu.

Deutschland Bayer Leverkusen - RB Leipzig
RB Leipzig yatafuta tikiti ya mchujoPicha: picture-alliance/dpa/M. Becker

Liverpool watakuwa ugenini dhidi ya Sevilla katika Kundi E, ambapo wataweza kufuzu kama watapa ushindi. Shakhtar wakati huo huo watasonga mbele pamoja na Manchester City – ambao watakuwa nyumbani dhidi ya Feyenoord – katika Kundi F kama wataepuka kichapo dhidi ya Napoli, ambao lazima washinde ili wawe na matumaini yoyote.

Besiktas watafuzu na kuongoza Kundi G kama watatoka sare na Porto, ambao watafuzu kama watapata ushindi. Monaco wataangushana na Leipzig, ambao wote watahitaji ushindi ili kuyaweka hai matumaini yao.

Manchester United watacheza na Basel katika Kundi A, na watahitaji sare tu ili kufuzu. Basel wanafahamu ushindi unaweza kuwapa tikiti kama CSKA watashindwa dhidi ya Benfica, nao Wareno hao lazima washinde na watumai kuwa Basel watachapwa.

Paris Saint-Germain watataraji kupata nafasi ya kwanza kwenye Kundi B kwa kuwagwangura Celtic, wakati Bayern, ambao tayari wamefuzu, wakicheza ugenini na Anderlecht.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman