Timu za Manchester zatamba England | Michezo | DW | 26.02.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Timu za Manchester zatamba England

Katika Ligi Kuu England Jumapili mechi iliyosubiriwa kwa hamu na mashabiki ilikuwa uwanjani Old Trafford ambapo wenyeji Manchester United walikuwa wanawaalika Chelsea.

Mshambuliaji wa United Romelu Lukaku aliwanyamazisha wale waliokuwa wanazungumzia uwezo wake wa kukucheza vyema dhidi ya timu mahiri kwa kuwa alifunga goli la kwanza la Manchester United na kuunda la pili lililotiwa kimiani na Jesse Lingard.

Chelsea walikuwa kifua mbele katika mechi hiyo kupitia Willian ila United walijizoazoa na kuebuka na ushindi mbele ya mashabiki wao na sasa wanaishikilia nafasi ya pili nyuma ya Manchester City katika jedwali la ligi ya nchini England huku Chelsea wakiwa wanaendelea kuyadidimiza matumaini yao ya kumaliza miongoni mwa timu nne bora.

Manchester City wao walikuwa wanacheza fainali ya taji la Carabao uwanjani Wembley dhidi ya Arsenal na walikuwa na kazi rahisi walipowapepeta tatu mtungi hao the gunners Sergio Aguero, nahodha Vincent Kompany na David Silva wakiwafungia City mabao yao na kumpa Pep Guardiola kikombe chake cha kwanza tangu kuchukua uongozi wa klabu hiyo.

Mwandishi: Jacob Safari/DPAE/Reuters

Mhariri: Josephat Charo