Timu kutafuta nafasi za mwisho za robo fainali | Michezo | DW | 13.03.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Timu kutafuta nafasi za mwisho za robo fainali

Atletico Madrid na Sevilla zinatarajia kuhakikisha kuwa Uhispania inawakilishwa na timu nne katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza

Barcelona walifanya muujiza na kufuzu pamoja na Real Madrid. Kwa misimu minne iliyopita, Uhispania imekuwa na timu tatu katika hatua ya nane za mwisho.

Atletico Madrid wako katika hali nzuri kabisa kabla ya kushuka dimbani siku ya Jumatano dhidi ya Bayer Leverkusen kwa mchuano wa marudiano. Vijana hao wa Diego Simeone wako kifua mbele kwa mabao 4-2.

Sevilla watakutana Jumanne na mabingwa wa England Leicester ambao wameanza kupata matokeo mazuri baada ya kutimuliwa kocha wao Claudio Ranieri. Leicester walifungwa 2-1 na Sevilla katika mkondo wa kwanza.

Manchester City watakuwa ugenini dhidi ya Monaco na watalenga kuendeleza mchezo wao mzuri kama waliocheza na kuwashinda Wafaransa hao 5-3 katika mkondo wa kwanza. Mabingwa wa Italia Juventus wanaangushana na Porto wakiwa na faida ya mabao 2-0 waliofunga mjini Lisbon

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com