Timu kumi za Afrika kushiriki mechi za mchujo | Michezo | DW | 05.11.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Timu kumi za Afrika kushiriki mechi za mchujo

Timu kumi zimeingia katika awamu ya mwisho ya kufuzu katika dimba la Kombe la Dunia nchini Brazil hapo mwakani, ambapo droo ya mechi za mchujo itafanywa na FIFA nchini Misri Septemba 6.

Cameroon iliizaba Libya bao moja kwa sifuri hapo jana na kujiunga na Misri, Cote d'Ivoire, Algeria, Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Ethiopia, Visiwa vya Cape Verde na Senegal katika awamu ya mchujo ambayo itaamuliwa kupitia droo itakayoandaliwa na FIFA katika makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika - CAF mjini Cairo, Misri mnamo Septemba 6.

Orodha ya timu za FIFA iliyotolewa Septemba 12 itatumiwa kuamua droo hiyo huku timu tano bora zikiwekwa katika kundi la kwanza na nyingine tano zikiwekwa katika kundi la pili. Kutakuwa pia na droo ya kuamua ni timu zipi zitaanza kwa kucheza nyumbani. Mechi hizo za nyumbani na ugenini zitachezwa mnamo Oktoba 11-15 katika mkondo wa kwanza na kati ya Novemba 15-19 kwa mechi za mkondo wa pili. Cote d'Ivoire, Ghana, Algeria, Nigeria na Visiwa vya Cape Verde ni miongoni mwa timu bora zotakazoorodheshwa katika awamu ya mchujo.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters/AFP/DPA

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman