Timu kujikatia tikiti ya 16 za mwisho | Michezo | DW | 21.11.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Timu kujikatia tikiti ya 16 za mwisho

Mabingwa watetezi Real Madrid, Barcelona, Manchester City na Juventus ni miongoni mwa timu zinazoweza kujikatia tikiti ya hatua ya 16 za mwisho katika michuano ya wiki hii ya makundi katika Champions League

Timu nyingine zinazosaka nafasi hiyo ni Bbenfica, Napoli, Besiktas, Monaco, Bayer Leverkusen, Leicester City, Porto na Sevilla. Timu tano tayari zimefuzu kwa hatua ya 16 za mwisho – Atletico Madrid, Bayern Munich, Borussia Dortmund, Arsenal na Paris St Germain watakaokabiliana Jumatano kutafuta uongozi wa Kundi A. Madrid wa pili katika Kundi F, pointi mbili nyuma ya Dortmund, watacheza nyumbani kwa Sporting Lisbon kesho. Dortmund watachapa dhidi ya Legia Warsaw.

Sevilla watawakabili Juventus kesho katika Kundi H, wakati Lyon itacheza na Dinamo Zagreb.

Viongozi wa Kundi C Barcelona watacheza na washika mkia Celtic wakati Manchester City watacheza dhidi ya Borussia Moenchengladbach, lakini ni Gladbach wanaohitaji ushindi sana dhidi ya City na Barcelona.

Atletico watakuana na PSV Eindhoven Jumatano, pointi tatu nyuma ya Bayern Munich katika kundi D. Bayern watacheza na Rostov.

Leicester itahitaji sare dhidi ya Club Brugge ili kufuzu, wakati Porto itapenya kwa ushindi dhidi ya FC Copenhagen.

Tottenham wanahitaji pointi tatu watakapocheza na viongozi wa Kundi E Monaco, ambao wanahitaji sare ili kufuzu na watatumai Bayer Leverkusen watakabwa na CSKA Moscow. Leverkusen itafuzu kama itaepuka kichapo nao Spurs wapoteze.

Vita vya kundi B vinaendelea ambapo Besiktasa itachuana na Benfica wakati Napoli itasakata na Dynamo Kiev.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef