Tikiti za kuingia makundi Champions League | Michezo | DW | 18.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Tikiti za kuingia makundi Champions League

Ufahari na fedha taslimu kwa kufuzu katika hatua ya makundi ya Champions League vinazisubiri timu kumi wakati duru ya kufuzu kwa tamasha hilo kubwa zaidi Ulaya ikifikia kilele katika wiki mbili zijazo

Lakini kama kuna shinikizo lolote linaloongozeka katika awamu hii ya mchujo ya mechi za mikondo miwili, Arsenal huwa haionyeshi hilo hata kidogo.

Klabu hiyo ya England inashiriki katika awamu hii kwa mara ya saba katika miaka tisa na imeshinda mechi zote 12 za awali, na kuimarisha rekodi yake ya kucheza katika hatua ya makundi ya Champions League tangu msimu wa 1998-99.

Arsenal wanashuka dimbani kesho ugenini dhidi ya Besiktas ya Uturuki, wakati Napoli wakiangushana na Athletic Bilbao. Celtic watakuwa nchini Slovenian kupmabana na NK Maribor siku ya Jumatano. Bayer Leverkusen watachuana na FC Copenhagen kesho. Zenit St. Petersburg wa Urusi watakuwa wageni wa Standard Liege nchini Ubelgiji siku ya Jumatano.

Katika mechi nyingine, za Jumatano, Aalborg vs. APOEL na Slovan Bratislava vs.BATE Borisov. Kesho Jumanne, Lille vs. FC Porto, Red Bull Salzburg vs. Malmo na Steaua Bucharest vs. Ludogorets Razgrad.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu