1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thomas Lubanga kuendelea kuzuiliwa

8 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EY32

THE HAGUE

Mahakama ya uhalifu wa kivita ya Mjini Tha Hague Uholanzi imefahamisha kwamba kiongozi wa zamani wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi wa Kongo Thomas Lubanga ataendelea kubakia kizuizini hadi yatakapotolewa matokeo kuhusu rufaa iliyofikishwa mbele ya mahakama na waendesha mashataka dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kumuachia huru mtuhimiwa huyo wa uhalifu wa kivita.Wiki iliyopita mahaka hiyo ya kimataifa ilipitisha uamuzi wa kuondolewa kizuizini bwana Lubanga kutokana na kucheleweshwa kwa kesi dhidi yake.Kesi hiyo ya uhalifu wa kivita ambayo ni ya kwanza katika mahakama hiyo ya ICC ilitakiwa kuanza wiki mbili zilizopita lakini ilikwama baada ya mahakama kupitisha uamuzi kuwa waendesha mashataka walizuia kimakosa ushahidi unaompendelea Lubanga kuwafikia mawakili wake.Mahakama ya The Hague imesema kesi hiyo huenda ikaanza mwezi Septemba. Lubanga mwenye umri wa miaka 47 anatuhumiwa kuhusika na visa vya utekaji nyara watoto chini ya umri wa miaka 15 na kuwaingiza kwenye jeshi la waasi mwezi septemba mwaka 2002 hadi mwezi Agosti mwaka 2003 katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.