THESSALONIKII:Polisi wapambana na waafrika wanaopinga kifo cha mwenzao nchini Ugiriki | Habari za Ulimwengu | DW | 21.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

THESSALONIKII:Polisi wapambana na waafrika wanaopinga kifo cha mwenzao nchini Ugiriki

Polisi wa Ugiriki wamepambana na wahamiaji wa kiafrika katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Thessaloniki waliyokuwa wakipinga mauaji ya mhamiaji wa kinigeria mwisho mwa wiki.

Kijana huyo wa Kinigeria alifariki baada ya kuruka kutoka kwenye jengo moja alikokuwa akiuza dvd zilizodurufiwa, baada ya kuhofu kuwa polisi walikuwa wakitaka kumkamata.

Hata hivyo polisi katika mji huo wamesema kuwa kulikuwa hakuna afisa yoyote wa polisi aliyetaka kumkamata.

Waandamanaji hao wakiwa na picha za mtu huyo walipambana na polisi ambao walilazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com