THE HAGUE:Waasi wa LRA huenda wasihukumiwe makubaliano ya amani yachangia | Habari za Ulimwengu | DW | 18.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

THE HAGUE:Waasi wa LRA huenda wasihukumiwe makubaliano ya amani yachangia

Makundi mawili ya kutetea haki za binadamu yanaonya kuwa wahusika wa uahlifu wa kivita nchini Uganda huenda wakaepuka kushtakiwa kufuata makubaliano kati ya serikali na waasi wa Lords Resistance Army LRA.

Serikali ya Uganda na waasi hao walifikia awamu ya tatu ya makubaliano mwishoni mwa mwezi uliopita yanayolenga kumaliza mgogoro wa miaka 20 kaskazini mwa Uganda.Vita hivyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuacha takriban milioni 2 bila makao.

Awamu hiyo ya tatu inatilia maanani uwajibikaji wa viongozi wa waasi hao wanaokabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Ghasia hizo nchini Uganda zimeendelea tangu mwaka 88 wakati kiongozi wa waasi wa LRA Joseph Kony alipochukua uongozi wa vuguvugu hilo.Kundi la LRA linadai kuwa linapigania kuanzishwa serikali inayofuata amri kumi na Biblia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com