1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE : Seselj kuzuiliwa asifariki kwa kugoma kula

7 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClv

Mahkama ya Uhalifu wa Vita ilioko The Hague nchini Uholanzi imewaamuru maafisa wa Uholanzi kutomruhusu kiongozi wa sera kali za kizalendo wa Serbia Vojislav Seselj kufa kutokana na mgomo wake wa kususia chakula.

Seselj mwenye umri wa miaka 52 anakabiliwa na mashtaka ya mauaji na mateso na amekuwa akikigomea chakula kwa siku 26.Mahkama hiyo imeamuru Seselj alishwe kwa kutumia mipira na msemaji wa mahkama amesema madaktari wana wasi wasi sana na afya yake.

Seselj alianza mgomo huo wa kula baada ya kupatiwa wakili alieteuliwa na mahkama wakati alipokataa kufika mahkamani katika siku ya kwanza ya kesi yake.