1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE : Mashtaka dhidi ya Lubanga yaanza kusikilizwa

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuO

Wawakilishi wa askari watoto wa zamani na waendesha mashtaka hapo jana wamewasilisha ushahidi kwa mara ya kwanza kabisa katika Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya kiongozi wa wanamgambo nchini Congo Thomas Lubanga.

Wakili wa waendesha mashtaka Ekkehard Withopf amesema Lubanga muasisi na kiongozi wa mojawapo wa wanamgambo walio hatari kabisa katika wilaya Ituri Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo aliwafunza watoto namna ya kuuwa,aliwafanya wauwe na wao wenyewe kuuwawa.

Amesema kwamba watawasilisha ushahidi kwamba kuna sababu za kutosha kuamini kwamba Lubanga mwenye umri wa miaka 45 ana hatia ya vitendo vya uhalifu anavyoshtakiwa.

Mahkama hiyo ya Kimataifa ya Uhalifu ilianzishwa hapo mwaka 2002 kuwashtaki watu binafsi na Lubanga anakuwa mtuhumiwa wa kwanza kufikishwa kwenye mahkama hiyo.