1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Martic amehukumiwa kifungo cha miaka 35

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsM

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Vitani mjini The Hague,imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 35 kwa kiongozi wa zamani wa Kiserbia kwa ukatili uliofanywa Croatia.Milan Martic amekutikana na hatia ya mauaji na mateso katika miaka ya tisini,wakati wa uongozi wake katika Jamhuri ya Serbia ya Krajinya iliyojitangazia yenyewe ambyo ilidumu kuanzia mwaka 1991 hadi 1995.Majaji wamesema,Martic ana hatia ya mauaji ya takasa takasa ya kikabila.Martic lakini amekataa mashtaka hayo.Martic pia amekutikana na hatia ya shambulizi la roketi dhidi ya mji mkuu wa Croatia,Zagreb.Shambulizi hilo,kijeshi,halikuwa na maana na liliua idadi kadhaa ya raia na kujeruhi mamia wengine.