1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Mahakama yaagiza waziri na kiongozi wa Janjaweed wakamatwe

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5A

Mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague imetoa agizo la kukamatwa waziri mmoja katika serikali ya Sudan na kiongozi wa kundi la Janjaweed wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.

Hata hivyo utawala wa Sudan umekataa kuwakamata watu hao na pia huenda watuhumiwa hao wakakosa kujisalimisha kwa hiari yao.

Kiongozi wa mashtaka wa mahakama hiyo ya kimataifa Luis Moreno Ocampo amesisitiza kuwa serikali ya Sudan inawajibika kisheria kuhusu kuwakamata watuhumiwa hao na kuwafikisha mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa.

Mnamo mwezi wa Februari, watuhumiwa hao wawili walitajwa kuhusiana na makosa 51 ya uhalifu wa kivita uliotendewa binadamu katika jimbo la Darfur.