1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Del Ponte aonya kuhusu uhusiano wa karibu na Serbia

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBo3

Mwendesha mashtaka mkuu wa uhalifu wa vitani wa Umoja wa Mataifa,ameuonya Umoja wa Ulaya dhidi ya kuanzisha uhusiano wa karibu na Serbia mpaka atakapokamatwa,mshukiwa mkuu kuhusika na uhalifu wa vitani.Carla Del Ponte amesema,matayarisho ya kuipokea Serbia katika Umoja wa Ulaya, yashughulikiwe tu kama Ratko Mladic,aliekuwa jemadari wakati wa vita,atafikishwa katika mahakama ya uhalifu wa vitani ya Umoja wa Mataifa mjini The Hague.Mladic anashtakiwa mauaji ya halaiki ya Waislamu 8,000 wa Bosnia katika mwaka 1995,katika mji wa Srebrenica.Washtakiwa wengine 3 wanaosakwa na mahakama ya The Hague,vile vile wapo mafichoni.