1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thatcher alazwa hospitali

Mohamed Dahman8 Machi 2008

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher yuko kwenye hali nzuri baada ya kulazwa hospitalini.

https://p.dw.com/p/DL5X
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret ThatcherPicha: DW-TV

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC Thatcher amefikishwa hospitali kusini mwa London hapo jana ili kufanyiwa uchunguzi wa tahadhari kwa kuchukuliwa vipimo vyake.

Msemaji wa hospitali ya St. Thomas mjini London ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba wamechukuwa vipimo vya Thatcher lakini hawatotowa habari zozote zile zaidi hadi hapo watakapokuwa wamezumgumza na katibu wake myeka.

Thatcher amekuwa akionekana hadharani kwa nadra katika miaka ya hivi karibuni baada ya kupigwa na kiharusi kidogo mfululizo hapo mwaka 2002 ambacho kilimlazimisha afute ratiba zake za mikutano ya hadhara.

Thatcher mwenye umri wa miaka 82 alikuwa waziri mkuu mwanamke wa kwanza nchini Uingereza ambapo aliongoza kwa zaidi ya muongo mmoja baada ya kuchaguliwa kwake hapo mwaka 1979 na kujipatia sifa ya kuwa mmojawapo ya wanasiasa wakakamavu kabisa katika enzi yake.