Tetemeko la ardhi nchini Chile. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.02.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Tetemeko la ardhi nchini Chile.

Watu 78 wafa baada ya Chile kutingiswa na tetemeko kubwa la ardhi.

default

Tetemeko la ardhi Chile, watu 78 wauawa.

Rais wa Chile Michelle Bachelet ametangaza hali ya kitaifa ya janga nchini humo baada ya watu 78 kuuawa  kufuatia tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha richta 8.8  kutokea nchini humo mapema leo. Majengo yaliporomoka katika mji mkuu, Santiago, kilomita 300 kutoka kitovu cha tetemeko hilo. Kulingana na Taasisi ya Jeologia ya Marekani, USSG kitovu cha Zilzala hiyo ilikuwa kilomita 90 kutoka mji wa Concepcion, mji mkuu wa pili nchini Chile.

Chile Erdbeben Februar 2010

Gari zapindukia kwa kishindo cha tetemko la ardhi.

Nchi za eneo la Pacific na mataifa yote 53, katika eneo la pwani ya Magharibi ya Kusini na Amerika ya Kati, yametoa onyo ya kutokea kwa dhoruba la Tsunami.

Onyo kama hilo pia limetolewa, nchini Japan, Australia na Alaska nchini Marekani.Ukilinganisha, tetemeko lililotokea kisiwani Haiti mwezi wa Januari  lilikuwa na ukubwa wa 7.0.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com