Tetemeko dogo la ardhi Uingereza
27 Februari 2008Matangazo
LONDON:
Tetemeko dogo la ardhi limetokea nchini Uingereza likiwa na nguvu ya 4.7 katika Kipimo cha Richter.Kwa hivi sasa hakuna ripoti za hasara iliyosababishwa lakini watu wengi katika mji mkuu London na kwengineko walishtushwa usingizini.
Kiini cha tetemeko hilo lilitokea muda mfupi baada ya usiku wa manane,kilikuwa kama kilomita 80 mashariki ya mji wa Sheffield kaskazini mwa Uingereza.