TEL AVIV:Olmert ndani ya mbinyo mkubwa | Habari za Ulimwengu | DW | 04.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEL AVIV:Olmert ndani ya mbinyo mkubwa

Inakadiriwa kiasi cha watu laki moja wameandamana hapo jana katika mji mkuu wa Israel Tel Aviv kumshinikiza Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ehud Olmert ajiuzulu.

Maandamano hayo yamekuja saa chache tu baada ya bunge kuanza mjadala juu ya hatima ya bwana Olmert kuendelea kuwa Waziri Mkuu wa Israel.

Pamoja na kutolewa kwa wito wa kujiuzulu kutoka upande wa upinzani, hakuna kura yoyote ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa.

Hali hiyo iliongezwa utambi siku ya jumatatu baada ya kutolewa ripoti, iliyoelezea jinsi serikali ya Olmert ilivyoshughulikia vita vya nchi hiyo na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon.

Hapo siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Tzipi Livni ambaye anatoka katika chama cha Bwana Olmert alimtaka Waziri Mkuu huyo ajiuzulu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com