TEL AVIV:Maandamano ya mashoga ya kila mwaka yaanza | Habari za Ulimwengu | DW | 08.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEL AVIV:Maandamano ya mashoga ya kila mwaka yaanza

Maelfu ya mashoga na wanaharakati wameandamana na kufanya sherhe katika maandamano ya kila mwaka ya mashoga mjini Tel Aviv.Washiriki walicheza na kusharabuka kutoka eneo la katikati la Rabin hadi ufuoni mwa bahari ambako tamasha maalum ziliandaliwa.

Kulingana na polisi takriban watu alfu 10 wanahudhuria sherehe hizo na hakuna visa vyovyote vilivyoripotiwa hata baada ya watu walio na misimamo mikali kutisha kuvuruga maandamano hayo yaliyoandaliwa na mji tangu mwaka 98.

Baadhi ya wanaopinga maandamano hayo walizuliwa na polisi lakini kuwatusi washiriki walipopita barabarani.Maandamano hayo yanafanyika siku mbili baada ya bunge kupitisha mswada utakaoruhusu baraza la mji wa Jerusalem kupinga maandamano ya aina hiyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com