TEL AVIV: Ehud Barak aidhinishwa kuwa waziri wa ulinzi, Israil | Habari za Ulimwengu | DW | 16.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEL AVIV: Ehud Barak aidhinishwa kuwa waziri wa ulinzi, Israil

Waziri Mkuu wa Israil, Ehud Olmert, amemwidhinisha kiongozi aliyechaguliwa hivi karibuni wa chama cha Leba kuwa waziri wa ulinzi.

Ehud Barak anachukua mahali pa Amir Peretz, aliyekuwa kiongozi wa chama hicho kabla ya kushindwa mapema juma hili.

Uteuzi wa Ehud Barak kuwa waziri wa ulinzi unatarajiwa kupitishwa bungeni Jumatatu ijayo.

Wakati wa harakati zake za kuwania uongozi wa chama cha Leba, Ehud Barak alikuwa amemtaka Ehud Olmert ajiuzulu kwa sababu ya vita vya msimu wa kiangazi uliopita dhidi ya wanamgambo wa Hizbullah nchini Lebanon.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com