TEHRAN : Wairan wako katika chaguzi mbili | Habari za Ulimwengu | DW | 15.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Wairan wako katika chaguzi mbili

Wananchi wa Iran leo wanapiga kura katika uchaguzi wa mabaraza ya serikali za mitaa na chombo muhimu chenye nguvu cha masheik kinachoitwa Baraza la Wataalamu.

Chaguzi hizo mbili ni majaribu ya kwanza kwa Rais Mahmoud Ahmadinejad tokea aliposhinda uchaguzi hapo mwaka jana.Uchaguzi wa mabaraza hayo ya miji na vijijini na Baraza la Wataalamu ambalo linahesabiwa kuwa ni taasisi yenye nguvu kubwa kabisa katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran zitaonyesha iwapo wapinzani wa Rais Ahmedinejad wanarudisha umashuhuri ijapokuwa matokeo ya chaguzi hizo hayana taathira ya moja kwa moja juu ya sera za nchi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com