TEHRAN: Iran yasema itaendelea na mradi wake wa kinyuklia hata ikiwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN: Iran yasema itaendelea na mradi wake wa kinyuklia hata ikiwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad amesema serikali yake itaendelea kushughulikia mradi wake wa nishati ya kinyuklia ingawa Umoja wa Mataifa unapinga.

Kwenye hotuba aliyotoa bungeni, Rais Mahmoud Ahmadinejad alisema hata kama Baraza la Usalama la Umoja huo litatangaza maazimio kumi kupinga mradi huo, Iran haitateteleka.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa lilipitisha azimio mwezi uliopita kuiwekea Iran vikwazo kwa kukataa kusitisha shughuli ya kurutubisha madini ya yuranium yanayotumika kutengeneza bomu la kinyuklia.

Iran imekuwa ikisisitiza kwamba mradi wake huo ni wa amani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com