1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran yaonya mataifa ya magharibi.

22 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGi

Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei ametoa onyo kwa mataifa ya magharibi kuwa nchi yake itapambana kwa kila uwezo iliyonayo iwapo itashambuliwa.

Katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya televisheni pia amesema kuwa Iran itajiingiza katika kile alichosema kuwa ni shughuli zilizo kinyume na sheria za kinuklia , iwapo umoja wa mataifa utasisitiza vikwazo vipya dhidi ya mpango wake wa kinuklia.

Hapo mapema waziri wa mambo ya kigeni wa Russia Sergei Lavrov amesema kuwa nchi yake haitaunga mkono kile alichokieleza kuwa vikwazo vya kupita kiasi dhidi ya Iran.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa hivi sasa linajadili muswada wa azimio ambao utaweka vikwazo zaidi dhidi ya Iran kuhusiana na mpango wake wa kinuklia.

Wanadiplomasia wa umoja wa mataifa wanasema kuwa wanatarajia kura itapigwa wiki ijayo kuhusiana na hatua hizo zilizopendekezwa, ikiwa ni pamoja na vikwazo kamili katika mauzo ya nje ya silaha ya Iran.