TEHRAN : Iran yaapa kujibu shambulio la Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Iran yaapa kujibu shambulio la Israel

Iran imeonya leo hii itamfanya adui yoyote yule ajutie shambulio dhidi ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran baada ya gazeti la Uingereza kurepoti kwamba Israel ilikuwa inapanga kushambulia mitambo ya nuklaa ya nchi hiyo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Mohammad Ali Hosseini amewaambia waandishi wa habari kwamba hatua yoyote ile dhidi ya Jamhuri hiyo ya Kiislam haitoachiliwa bila ya kijibiwa na kwamba mchokozi atajutia kitendo chake hicho kwa haraka sana.

Afisa mwandamizi wa serikali ya Israel ametupuilia mbali kuwa ni upuuzi repoti za gazeti la The Sunday Times kwamba taifa hilo la Kiyahudi lilikuwa limeandaa mipango ya kuteketeza mitambo ya kurutubisha uranium kwa shambulio la mbinu maalum la nuklea.

Hussein amesema hali hiyo inakuja kufuatia kukiri kwa Waziri Mkuu wa Israel ambaye aliungama kwamba utawala wa Israel unamiliki silaha za nuklea kwa kile kinachoonekana kama kuteleza ulimi kwa Ehud Olmert hapo mwaka jana ambako kulivunja ukimya wa serikali uliodumu kwa miongo kadhaa juu ya mipango ya nuklea ya Israel.

Israel inaiona Iran kuwa adui yake mkubwa kutokana na wito wa mara kwa mara wa Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran wa kutaka Israel kufutwa kwenye ramani ya dunia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com