1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Haniyah asema katu chama chake hakitatambua Israel.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClN

Waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh , ambaye hivi sasa yuko ziarani nchini Iran , amesema kuwa serikali yake inayoongozwa na chama cha Hamas haitatambua haki ya Israel kuwapo. Akizungumza na maelfu ya waumini baada ya sala ya Ijumaa katika chuo kikuu cha Tehran , amesema kuwa Hamas kitaendelea na mapambano yake kuukomboa mji wa Jerusalem. Upinzani wa serikali yake kuhusu suala hilo umepelekea umoja wa Ulaya na Marekani kusitisha misaada yake kwa Wapalestina.

Tangu wakati huo Iran imeongeza kwa kiasi kikubwa msaada wake wa kifedha kwa mamlaka hiyo ya Palestina.