TBILISI: Rais wa Georgia aitisha uchaguzi mapema | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TBILISI: Rais wa Georgia aitisha uchaguzi mapema

Rais wa Georgia,Mikhail Saakashvili amesema, uchaguzi wa rais utafanywa mapema na utakuwa kabla ya mwezi wa Januari.Akaongezea kuwa hali ya hatari iliyotangazwa siku ya Jumatano baada ya maandamano kuvunjwa na polisi wa kuzuia ghasia, itaondoshwa hivi karibuni.Hata hivyo viongozi wawili wa upinzani wametiwa mbaroni kwa tuhuma ya kuhusika na mawakala wa Kirusi na kupanga njama ya kutaka kuipindua serikali.

Kwa upande mwingine,Marekani tena imetoa mwito wa kuiondosha haraka amri ya hali ya hatari iliyotangazwa nchini Georgia.Na kuhusu stehseni za redio na televisheni zilizofungwa,Washington imesema,vyombo vya habari lazima viruhusiwe kufanya kazi bila ya vizingiti.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com