1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taylor asusia ufunguzi wa kesi yake mjini The Hague

Sekione Kitojo4 Juni 2007

Kesi ya rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor , anayetuhumiwa kwa kufadhili kundi la waasi katika nchi jirani ya Sierra Leone, kundi ambalo lilifanya unyama katika kampeni yao iliyogharamiwa na biashara ya mauzo ya almasi kwa kufanya ubakaji, na kuwakata viungo vya mwili watu kadha , imeanza leo kwa mvutano na wakili wa Taylor kutoka nje ya mahakama akionyesha malalamiko ya mteja wake kuwa hakutendewa haki.

https://p.dw.com/p/CB3o
Mahakama maalum ya umoja wa mataifa kuhusu Sierra Leone inayomhukumu Charles Taylor mjini The Hague.
Mahakama maalum ya umoja wa mataifa kuhusu Sierra Leone inayomhukumu Charles Taylor mjini The Hague.Picha: AP

Kiongozi huyo wa kwanza wa taifa la Kiafrika alitarajiwa kusimama kizimbani kujibu tuhuma za uhalifu wa kivita mbele ya mahakama ya kimataifa , Charles Taylor , alitarajiwa kuwa mbele ya mahakama maalum inayoungwa mkono na umoja wa mataifa kuhusiana na Sierra Leone.

Kesi hiyo ilianza saa nne na nusu kwa saa za Ulaya ya kati mjini The Hague ambako mahakama hiyo inayohusu Sierra Leone ilihamishiwa baada ya maafisa kuamua inawezekana kutokea ghasia iwapo kesi hiyo ingefanyika mjini Freetown, nchini Sierra Leone.

Taylor mwenye umri wa miaka 59, anakabiliwa na mashtaka 11 ya uhalifu dhidi ya ubinadamu pamoja na uhalifu wa kivita makosa yaliyotendwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone mwaka 1991 hadi 2001 , vita vinavyojulikana kuwa vya kinyama zaidi katika historia. Zaidi ya watu 200,000 wameuwawa katika mapigano hayo na waasi waliwakata viungo vya miili watu zaidi ya laki moja, wakiwakata mikono, miguu, masikio na pua.

Wakati wa kuanza kwa kesi hiyo kulitokea mvutano kati ya jaji Julie Sebutinde na wakili wa Taylor kuhusiana na kutokuwepo mteja wake mahakamani.

Rais huyo wa zamani wa Liberia Charles Taylor amesusia ufunguzi wa kesi hiyo, akilalamika kuwa haamini iwapo itapewa haki. Katika barua kwa mahakama hiyo na kusomwa na wakili wake , Taylor amesema amezuiwa kumuona wakili wake na kwamba wakili aliyeteuliwa na mahakama kumuwakilisha amekuwa hatoshi pekee ikilinganishwa na kundi la wanasheria wa upande wa mashtaka.

Nasikitika sana kuwa sitoweza kuhudhuria vikao vya vyovyote vya kesi hii , Taylor amesema katika taarifa iliyosomwa na wakili wake Karim Khan.

Katika wakati fulani nilikuwa na imani na mahakama hii juu ya uwezo wa kupatikana haki. Lakini kwa muda sasa , imeonekana wazi kuwa uwezo huo umepotea, Taylor amesema katika taarifa yake.

Mwendesha mashtaka mkuu Stephen Rapp amepingana na madai hayo ya Taylor kuwa hana kikosi imara cha mawakili , na kwamba Taylor amepatiwa wakili , mchunguzi maalum pamoja na fedha.

Wakili wa Taylor hata hivyo alifikia kuvutana sana na jaji Sebutinde na hadi kuamua kutoka nje ya mahakama akipinda jinsi mteja wake anavyokandamizwa kisheria. Karim Khan amesema kuwa Taylor ameondoa ruhsa ya yeye kumuwakilisha mahakamani hapo na anafanya mipango ya kujiwakilisha binafsi. Khan hatimaye alikusanya mafaili yake na kutoka mahakamani. Mahakama hiyo iliamuru kesi kuendelea , na mwendesha mashtaka mkuu Stephen Rapp alianza kutoa taarifa yake ya mwanzo.

Jaji Sebutinde alimteua mtu mwingine mahakamani kumwakilishi Taylor.