Tarek Aziz afikishwa mahakamani | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Tarek Aziz afikishwa mahakamani

Kesi dhidi ya kitambulisho cha zamani cha utawala wa Sadam Hussein yafunguliwa jioni hii mjiini Baghdad

default

Tarek Aziz akihojiwa kama shahidi mwaka 2005Makamo wa zamani wa waziri mkuu wa Irak,alioyekua pia waziri wa mambo ya nchi za nje,kitambulisho cha utawala wa Sadam Hussein,Tarek Aziz,anafikishwa mahakamani hii leo kwa madai ya kuhusika na mauwaji ya wafanyabiashara kadhaa mnamo mwaka 1992.


Kesi hiyo iliyokua ianze kusikilizwa leo asubuhi imeakhirishwa hadi jioni.


Wafanyabiashara zaidi ya 40 walituhumiwa kupandisha bei za bidhaa muhimu kwa raia,wakikiuka viwango vya bei vilivyowekwa na serikali katika wakati ambapo Irak ilikua ikisumbuliwa na vikwazo vya Umoja wa mataifa vilivyowekwa baada ya kuivamia Kuweit mnamo mwaka 1990.


Wakili wa Tarek Aziz anasema madai dhidi ya mteja wake hayana msingi.


Tarek Aziz,mkristo pekee katika kundi la mwanzo la wakaribu wa Sadam Hussein,aliangaliwa na vyombo vya habari vya kimataifa kama kitambulisho cha utawala wa Irak,Kuweit ilipovamiwa na pia katika vita vilivyofuatia.


Alipokua waziri wa mambo ya nchi za nje,alichangia pakubwa katika jukwaa la kidiplomasia kabla ya vita vya kwanza vya Ghuba kuripuka,kutokana na fasaha yake katika kuzungumza lugha ya kiengereza ,subira na werevu wa kuongoza majadiliano.


Tarek Aziz atafika mbele ya mahakama kuu pamoja na washtakiwa wengine 7.Miongoni mwao wanakutikana nduguze Sadam Hussein-Ouatban Ibrahim al Hassan,aliyekua waziri wa mambo ya ndani mauwaji hayo yalipotokea na Sabaaoui Ibrahim al Hassan, aliyekua afisa wa ngazi ya juu wa usalama wakati ule.


Waziri wa zamani wa biashara na gavana wa benki kuu ni miongoni pia mwa washtakiwa.

"Mashtaka dhidi ya Tarek Aziz hayana ukweli wowote" amesema wakili wake Badia Arif.


"Upande wa mashtaka unachukulia tuu kwavile alikua mwanachama wa baraza la uongozi wa mapinduzi,lililopitisha amri ya kuuliwa wafanyabiashara hao,anabeba dhamana."Amelalamika wakili wake Badia Arif.


Miongoni mwa washtakiwa anakutikana pia binamu wa Sadam Hussein,Ali Hassan al Madjid mashuhuri kwa jina la "Ali kemikali.Madjid amehukumiwa adhabu ya kifo June mwaka jana kwa kushiriki katika opereshini ya kijeshi ya Anfar,ambapo maelefu ya wakurd waliuliwa katika mwaka 1980.


Mahakama kuu ya Irak imeundwa kuwahukumu wanaachama wa utawala wa zamani wa Sadam Hussein.


Tarek Aziz anaesemekana ni mgonjwa,ameshawahi kuhojiwa kama shahidi katika kesi kadhaa dhidi ya viongozi wa zamani wa Irak.


Kuwepo mkristo huyo katika serikali ya Sadam Hussein ndiko kulikokua kukitajwa kama ushahidi wa kuvumiliana waumini wa dini tofauti nchini Irak wakati ule.


Tarek Aziz alijisalimisha kwa vikosi vya Marekani April mwaka 2003,,wiki mbili tuu baada ya utawala wa Sadam Hussein kupinduliwa.

►◄

 • Tarehe 29.04.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DqZ6
 • Tarehe 29.04.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DqZ6
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com