Tanzania: Suala la Zanzibar ni nchi au si nchi | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Tanzania: Suala la Zanzibar ni nchi au si nchi

Nchini Tanzania, kumezuka sintofahamu juu ya suala la Zanzibar kuwa ni nchi au si nchi.

Bandari ya Zanzibar

Bandari ya Zanzibar

Sintofahamu hiyo ilikuja baada ya waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kusema ya kwamba Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya muungano.

Kauli yake hiyo ilizusha mjadala mkali katika baraza la wawakilishi huko Zanzibar ambapo mwanasheria mkuu wa wa huko Pandu Amir Kificho alitoa ufafanuzi kuwa Zanzibar ni nchi na kwamba Waziri Mkuu wa muungano aliteleza.

Aboubakary Liongo amewasiliana na Waziri wa nchi katika ofisi ya waziri mkuu anayeshughulika na masuala ya muungano Bw. Mohamed Seif Khatib ili kupata ufafanuzi juu ya suala hilo.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com