Tanzania: Miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.04.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Tanzania: Miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Watanzania leo, April 26, wanaadhimisha miaka 46 tangu kuundwa Muungano wa zilizokuwa dola huru za Tanganyika na Visiwa vya Zanzibar, hivyo kuzaliwa kwa taifa jipya la Tanzania.

default

Jiji la Dar es Salaam,Tanzania

Tokeo hilo lilifanyika wakati wa kusisimua katika siasa za Bara la Afrika, punde baada ya nchi nyingi za Afrika kupata uhuru, na miezi mitatu tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Mmoja kati ya mashahidi wa kuzaliwa Muungano huo ni Job Lusinde, waziri katika serikali ya Tanganyika punde baada ya uhuru mwaka 1961, na pia aliitumikia serikali ya Muungano.

Sansibar Stonetown

Mji Mkongwe wa Zanzibar,Tanzania

Othman Miraji amezungumza na Bw Job Lusinde huko kwake Dodoma na kwanza kumuuliza nini kilichowachochea waasisi wa Muungano huo, marais wa Tanganyika na Zanzibar, Julius Nyerere na Abeid Karume kuja na wazo hilo:

Mahojiano: Othman Miraji/Job Lusinde

Mpitiaji:Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com