1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TAMPERE.Mazungumzo na Uturuki juu ya kufungua bandari zake kwa Cyprus yamesambaratika

28 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCon

Finland ambayo ndio inashikilia urais unaozunguka wa nchi za umoja wa ulaya imesema kwamba mazungumzo na Uturuki kuhusu kufungua bandari zake na viwanja vya ndege kwa Cyprus inayotawaliwa na Ugiriki yamekwama.

Waziri wa mambo ya nje wa Finland Errki Tuomioja amezihimiza nchi 25 wanachama wa umoja wa ulaya kusimamisha mazungumzo na Uturuki kuhusu kujiunga na umoja huo.

Mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa ulaya watakutana Desemba tarehe 11 kuamua juu ya swala hilo.

Kumekuwa na mivutano juu ya sehemu mbili za kusini mwa Cyprus inayotawaliwa na Ugiriki ambayo ni mwanachama wa umoja wa ulaya na sehemu ya kaskazini mwa Cyprus iliyo chini ya Uturuki tangu ilipoivamia mwaka 1974.

Uturuki inadai kwanza lazima umoja wa ulaya utimize ahadi yake ya kuondoa vikwazo dhidi ya eneo hilo la Cyprus Kaskazini kabla ya makubaliano ya forodha kutiliwa maanani.