Tamaduni mbalimbali nchini Ujerumani ? | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 17.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Tamaduni mbalimbali nchini Ujerumani ?

Kansela Merkel amesema juhudi za kuleta utangamano wa tamaduni mbalimbali nchini Ujerumani zimeshindikana kabisa.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

POTSDAM:
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema juhudi za kuwaleta pamoja watu wa tamaduni mbalimbali nchini Ujerumani zimeshindikana kabisa.

Kansela Merkel aliyasema hayo mjini Potsdam kwenye mkutano wa tawi la vijana la chama chake cha kihafidhina CDU . Ameeleza kuwa itakuwa vigumu kuyafuta makosa yaliyofanyika kwa muda wa miaka mingi iliyopita.Kiongozi huyo wa Ujerumani pia ametahadharisha dhidi ya kuhimiza uhamiaji bila ya kufanya matayarisho ya kutosha.Ameeleza kuwa haipasi kusalimu amri mbele ya mwito wa kuhimiza uhamiaji wa kiwango kikubwa bila ya kwanza kufanya kila linalopasa kujenga uwezo wa wananchi wazaliwa na kuwapa fursa.

Kansela Merkel pia amesisitiza kwamba wahamiaji wanapaswa kujijumuisha na jamii na wajifunze lugha ya Kijerumani,lakini pia amesema anatambua umuhimu wa wahamiaji katika maendeleo ya uchumi wa Ujerumani.

 • Tarehe 17.10.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Pg83
 • Tarehe 17.10.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Pg83
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com