1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taharuki yatanda mpaka wa Isiolo na Samburu

9 Julai 2021

Hali ya Taharuki imetanda katika mipaka ya majimbo ya Isiolo na Samburu yaliyoko kaskazini mwa Kenya, baada ya makabiliano mapya kuzuka baina ya jamii hizo.

https://p.dw.com/p/3wGSQ
Kenia Camelmilk - Ole Nkiu standing with one of his camels
Picha: Jeroen van Loon

Kimya kisicho cha kawaida kinachanganyikana na wingu la hofu, kinachovunjwa na nyimbo za ndege, walioko kwenye majani ya miti…Birds/ Chirping…Chini ya mti, kikundi cha wazee wa kike na kiume wameketi mduara  wakijadili hali ya usalama katika eneo hili la Merti.

Kwa kipindi cha miezi sita iliyopita, makabiliano makali baina ya jamii zinazoishi kwenye mpaka kati ya majimbo ya Isiolo na Samburu yamekuwa yakishuhudiwa. Matokeo yake yamekuwa maafa, na wizi wa mifugo huku wakazi wakiishi kwa hofu na wasiwasi.

Wakazi wa Isiolo wanadai majirani zao walikuwa wamewaleta mifugo wao kwenye eneo la la malisho ndipo makabiliano yakaanza. Galacha Waario, mwenye umri wa miaka 63, alijeruhiwa kwenye makabiliano hayo, alipokuwa akichunga mifugo wake. Alipoteza mbuzi wake 200, walioibwa.

Mzee Galacha aliye na wake wawili na watoto 12 kwa sasa hana chochote baada ya utajiri wake kuibiwa huku akilazimika kugharamia matibabu kwa pesa nyingi.  Anasema kuwa kama mtu aliyetegemea ufugaji, kwa sasa hana uwezo wa kukimu familia yake kubwa. Anashikilia kuwa viongozi pamoja na serikali wamefeli kuwahakikishia usalama wao. Osman Abdi ni mwenyekiti wa baraza la Wazee hapa.

Matamshi ya viongozi hao yanajiri baada ya watu watano kuwaua katika mpaka wa majimbo ya Isiolo na Wajir baada ya wavamizi kushambulia. Kamishna wa kaunti ya Isiolo Herman Shambi alithibitisha shambulizi hilo lililotekelezwa mapema na asubuhi. Uchunguzi wa awali ukiyahusisha na mzozo wa maji na maeneo ya malisho.  Aidha kisa hicho kinajiri chini ya juma moja baada ya watu wengine sita kuuawa katika eneo hilo wakati wafugaji wa jamii ya Waturkana na Wasamburu walipokabiliana. Hassan Odha ni mbunge wa Isiolo Kaskazini.

Kwa muda sasa eneo hili limesalia kuwa na uwanja wa mapambano katika ya jamii za wafugaji, baada ya serikali ya mkoloni na serikali zilzotangulia kupatenga. Kutengwa huko kunatokana na kuwa ni eneo lenye ukavu na lisilo na idadi kubwa ya watu. Polisi wamepelekwa katika eneo hilo kuboresha usalama.

Wazee wa jamii hii wanapokongamana kutafuta suluhisho kwa utepetevu wa usalama katika eneo hili pana la Kaskazini mwa Kenya, ombi lao ni kwa wizara ya usalama wa taifa kutafuta mikakati ya kudumua ya kudumisha usalama.

Shisia Wasilwa, DW, katika jimbo la Isiolo, Kenya