1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yatishia kuvunja uhusiano wake wa kibalozi na Ufaransa

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjTQ

DAMASCUS:

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Syria-Walid Muallem- amesema kuwa nchi yake itavunja uhusiano wake wa kibalozi na Ufaransa kutokana na mgogoro wa kisiasa nchini Lebanon.

Tangazo hilo limekuja siku tatu baada ya rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kusimamisha mawasiliano na Syria kuhusu madai ya kuwa Damascus inazuia njia za kupata ufumbuzi wa kisiasa nchini Lebanon.Pande zote husika nchini Lebanoni-Serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi pamoja na upande wa upinzani unaonga mkono Syria zimeshindwa kupata ufumbuzi wa nani atakae chukua nafasi ya rais Emil Lahoud anaegemea upande wa Syria.Lahoud alijiuzulu wakati mda wake wa kutawala ulipomalizika Novemba 23.