Syria yasema iko tayari kwa mazungumzo na Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 09.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Syria yasema iko tayari kwa mazungumzo na Israel

DUBAI:

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Syria amesema kuwa nchi yake iko tayari kuhuisha mazungumzo ya amani na Israel.

Waziri huyo, Walid Muallem,katika mahojiano na kituo cha Televisheni ya kiarabu cha Al-Arabiya, amesema kuwa Syria iko tayari kwa mazungumzo na Israel, lakini akapinga hatua ya kijeshi kumaliza migogoro.

Mara ya mwisho nchi hizo mbili kufanya mazungumzo ulikuwa mwaka wa 2000.Mazungumzo yalitibuka baada ya kutokubaliana kuhusu milima ya Golan ambayo ilitekwa na Israel mwaka wa 1967 na kuyageuza sehemu yake mwaka wa 1981.

Viongozi wa Israel na Syria walisema mwaka jana kuwa wako tayari kuanza tena mazungumzo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com